Kipengele cha Jumbe Zenye Nyota kinakuruhusu kuziwekea ala jumbe maalum ili uweze kuzirejea tena baadaye.
Kuweka nyota kwenye ujumbe
- Gusa na shikilia ujumbe unaotaka kuuwekea nyota.
- Gusa ikoni ya
Nyota kwenye menyu inayotokea.

Kuondoa nyota kwenye ujumbe
- Gusa na shikilia ujumbe wenye nyota.
- Gusa ikoni ya
Nyota.
Kuangalia orodha ya jumbe ulizoweka nyota
- Fungua soga iliyo na jumbe zenye nyota unazotaka kuona.
- Gusa jina la soga.
- Gusa Jumbe zenye nyota.
Kuangalia Jumbe zote Zenye Nyota, nenda Mipangilio ya WhatsApp > Jumbe Zenye Nyota.
Jifunze jinsi ya kutumia kipengele cha Jumbe Zenye Nyota kwenye: Android | Windows Phone