Kipengele cha Jibu kinakuruhusu kujibu ujumbe fulani kwenye soga ya kibinafsi au kikundi.
Kujibu ujumbe:
- Android: Gusa na shikilia ujumbe, halafu gusa Jibu
. Andika jibu lako na gusa Tuma
.
- Mbadala, telezesha kulia kwenye ujumbe kujibu.
- Kujibu kibinafsi kwa mtu aliye kutumia ujumbe kwenye kikundi, gusa na shikilia ujumbe, kisha gusa Hiari Zaidi
> Jibu kibinafsi.
- iPhone: Gusa na shikilia ujumbe, halafu gusa Jibu
. Andika jibu lako na gusa Tuma
.
- Mbadala, telezesha kulia kwenye ujumbe kujibu.
- Kujibu kibinafsi kwa mtu aliye kutumia ujumbe kwenye kikundi, gusa na shikilia ujumbe, kisha gusa Zaidi
> Jibu kibinafsi
.
- Windows Phone: Bonyeza ujumbe kwa muda, halafu gusa jibu. Andika jibu lako na gusa tuma
.
- Kujibu kibinafsi kwa mtu aliye kutumia ujumbe kwenye kikundi, gusa na shikilia ujumbe, kisha gusa jibu kibinafsi.
- WhatsApp Web na WhatsApp Desktop: Vinjari juu ya ujumbe, halafu bofya Menyu
> Jibu. Andika jibu lako na bofya Tuma (
au
).
- Kujibu kibinafsi kwa mtu aliye kutumia ujumbe kwenye kikundi, vinjari juu ya ujumbe, halafu bofya ujumbe, kisha bofya Menyu
> Jibu kibinafsi.
Kumbuka: Ukitaka kusitisha jibu kabla ya kutuma, gusa au bofya “x” iliopo upande wa kulia wa ujumbe.