Bofya Menyu ( au ) juu ya orodha ya soga kwenye WhatsApp.
Mbadala, bofya ikoni ya Soga mpya.
Bofya Kikundi kipya.
Watafute au chagua waasiliani wa kuongeza kwenye kikundi. Kisha bofya mshale wa kijani.
Ingiza mada ya kikundi. Hii itakuwa jina la kikundi ambacho washiriki wote wataliona.
Kikomo cha mada ni herufi 25.
Unaweza kuongeza emoji kwenye mada kwa kubofya ikoni ya Emoji.
Kwa hiari, ongeza ikoni ya kikundi kwa kubofya ONGEZA IKONI YA KIKUNDI. Unaweza kuchagua Piga picha, Pakia picha au Tafuta Mtandaonikuongeza picha. Ukishaweka, ikoni itaonekana karibu na kikundi kwenye orodha ya soga zako.
Bofya alama hakikishi ya kijani unapomaliza.
Kualika kwa vikundi kwa kupitia viungo
Ukiwa mtawala wa kikundi, unaweza kuwaalika watu kujiunga na kikundi kwa kushirikisha kiungo nao. Kushirikisha kiungo cha mwaliko wa kikundi:
fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada ya kikundi.
Mbadala, bofya Menyu ( au ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
Bofya Alika kwa kikundi kwa kutumia kiungo.
Chagua Tuma Kiungo kupitia WhatsApp au Nakili Kiungo.
Ikiwa unatuma kwa kupitia WhatsApp, tafuta au chagua waasiliani, kisha bofya Tuma.
Mtawala anaweza Kutangua kiungo wakati wowote kufanya kiungo cha awali cha mwaliko batili na kuunda kiungo kipya.
Kumbuka: Mtumiaji yeyote wa WhatsApp unaye mshirikishia kiungo cha mwaliko anaweza kujiunga na kikundi, kwa hivyo tumia kipengele hiki tu na watu wanaoaminika. Inawezekana kwa mtu kusambaza kiungo kwa watu wengine. Ikiwa hivyo, watu hao wengine wanaweza pia kujiunga na kikundi na mtawala wa kikundi hataulizwa kuwaidhinisha watu hao kabla ya kujiunga.