Haiwezi kupokea arifa kwenye Opera
Ikiwa hupokei arifa kwenye mtandao wa WhatsApp, hakikisha arifa zako zimewashwa kwenye kivinjari chako.
Washa arifa
- Kwenye kivinjari chako, bofya Washa arifa kwenye desktop iliyopo kwenye bendera ya bluu juu ya orodha yako ya soga.
- Fuata maagizo kwenye skrini.
Dondoo: Ikiwa huoni bendera ya bluu, washa upya ukurasa. Ikiwa bado huoni bendera, huenda umetuliza au kuzima arifa kutoka kwenye mipangilio ya WhatsApp.
Ruhusu arifa
- Kwenye kivinjari chako, bofya ikoni ya Usanidi Rahisi > Nenda kwa mipangilio ya kivinjari.
- Mbadala, bofya Opera > Mipangilio.
- Bofya Mahiri > Faragha & Usalama > Mipangilio ya Tovuti > Arifa.
- Ikiwa “https://web.whatsapp.com” iko chini ya orodha ya Zuia bofya ikoni ya Zaidi karibu na > Ruhusu.
Mbadala, bofya ikoni ya kufunga kwa "web.whatsapp.com". Ikiwa kunjuzi ya Arifa imewekwa kuwa Zuia, badilisha iwe Ruhusu.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kubadili arifa kwenye WhatsApp Web au Desktop
- Haiwezi kupokea arifa: Chrome | Firefox | Microsoft Edge | Safari