Haiwezi kupokea arifa kwenye Firefox
Ikiwa hupokei arifa kwenye WhatsApp Web, hakikisha umewasha upokeaji wa arifa kwenye kivinjari chako.
Kuwasha arifa
- Kwenye kivinjari chako, bofya Washa arifa kwenye eneokazi, fanya hivyo kwenye bendera ya bluu juu ya orodha yako ya soga.
- Fuata maagizo kwenye skrini.
Kumbuka: Ikiwa huoni bendera ya bluu, pakia ukurasa upya. Ikiwa bado huoni bendera, huenda umesitisha au umezima arifa kwenye mipangilio yako ya WhatsApp.
Kuruhusu arifa
- Kwenye kivinjari chako, bofya aikoni ya Menyu, kisha bofya Chaguo au Mapendeleo.
- Bofya Faragha na Usalama.
- Chini ya Ruhusa, bofya Mipangilio… karibu na Arifa.
- Kama menyu kunjuzi ya "web.whatsapp.com" imewekwa kwenye Zuia, ibadilishe iwe Ruhusu.
- Bofya Hifadhi Mabadiliko.
Au, bofya aikoni ya kufuli karibu na "https://web.whatsapp.com/". Kama Tuma Arifa inaonyesha ikiwa Imezuiwa, bofya "x", kisha upakie ukurasa upya.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kubadilisha arifa kwenye WhatsApp Web au Desktop
- Huwezi kupokea arifa: Chrome | Microsoft Edge | Opera | Safari