Matatizo ya muunganisho kwenye simu yako, kompyuta au Wi-Fi ni baadhi ya sababu za kawaida za kushindwa kutuma au kupokea jumbe kwenye WhatsApp Web au Desktop.
Kama huwezi kutuma au kupokea jumbe kwenye WhatsApp ya simu yako, basi hutaweza kutumia WhatsApp Web au Desktop kwenye kompyuta yako. Fungua WhatsApp kwenye simu yako na jaribu kutuma ujumbe. Kama unashindwa, jifunze zaidi jinsi unavyoweza kutatua muunganisho wa simu yako: Android | iPhone
Kama unaweza kutuma ujumbe wa WhatsApp kutoka kwa simu yako, jaribu tena kutumia WhatsApp Web au Desktop kwenye kompyuta yako. Ikiwa bado una matatizo kutuma au kupokea ujumbe, kuna uwezekano kuwa una tatizo la muunganisho kwenye kompyuta yako.
Lazima uwe muunganisho wa Intaneti wenye nguvu na imara katika kompyuta yako kutumia WhatsApp Web au Desktop. Kama ukiona kibao cha njano juu ya orodha ya soga na ujumbe huu wa kosa "Kompyuta haijaunganishwa", angalia kuhakikisha muunganisho wa Intaneti wa kompyuta yako ni amilifu. Kama muunganisho wa intaneti ya kompyuta yako unafanya kazi kawaida na bado huwezi kutuma au kupokea jumbe, anzisha upya ukurasa kama upo kwenye WhatsApp Web au toka na uanzishe programu upya kama unatumia WhatsApp Desktop.
Kama tatizo linaendelea, jaribu kutoka na kuingia tena kwenye WhatsApp Web au Desktop, unaweza jifunza namna ya kufanya hivyo kwenye makala hii.
Dondoo: Kwa WhatsApp Web, lazima utumie sasisho la hivi karibuni la Chrome, Firefox, Microsoft Edge, Opera, au Safari. Vivinjari vingine kama vile Internet Explorer haviwezeshwi.
Kama unatumia mtandao uliosimamiwa wa Wi-Fi, kama vile ofisini,kwenye maktaba au chuo kikuu, mtandao wako huenda umesanidiwa kuzuia au kupunguza miunganisho kwenye WhatsApp Web. Ikiwa WhatsApp Web inakuarifu kuwa upo kwenye mtandao wa Wi-Fi unaozuia WhatsApp Web kufanya kazi kwa usahihi, tafadhali hakikisha mtandao wako umewekwa kupitisha trafiki kwenye "web.whatsapp.com", ".web.whatsapp.com", au ".whatsapp.net".