Je, kwa nini ninaona onyo la uthibitisho kutofaulu?
Code Verify huongeza safu ya ziada ya usalama kwenye ufumbaji wa mwisho hadi mwisho wakati watu wanatumia WhatsApp kwenye wavuti. Ikiwa umepakua kiendelezi cha kivinjari cha Code Verify, unaweza kuona onyo linalosema “Imeshindwa Kuthibitisha”. Hali hii inaweza kutokea kwa sababu zifuatazo:
- Una kiendelezi kingine kilichosakinishwa ambacho kinatatiza uwezo wetu wa kuthibitisha ukurasa.
- Msimbo unaoendesha ukurasa wako wa WhatsApp Web haulingani na msimbo ambao watu wengine wote wanaitumia.
- Hitilafu fulani imetokea upande wetu.
Ili kutatua tatizo hilo:
- Jaribu kusitisha viendelezi vyako vingine, kufanya mchakato wa uthibitishaji tena na kuendelea kutumia viendelezi vyako vingine baada ya kumaliza. Huenda itakubidi upakie upya WhatsApp Web ili kufuta onyo hili.
- Angalia uone kama suala limeshughulikiwa hadharani kwenye tovuti ya Uhandisi ya Meta au kwenye ukurasa wa Twitter wa Uhandisi wa Meta.
- Ikiwa halijashughulikiwa kuwa ni suala linalojulikana, ondoka kwenye akaunti yako ya WhatsApp Web na utumie WhatsApp kwenye kifaa chako cha mkononi, kwa kuwa ujumbe wako kwenye wavuti huenda usiwe wa faragha tena. Ikiwa ungependa kuchunguza suala hilo zaidi, bofya onyo jekundu la kushindika na upakue chanzo cha msimbo.
Rasilimali zinazohusiana:
- Kuhusu Code Verify
- Kwa nini ninaona hitilafu ya kuisha kwa muda wa mtandao?
- Kwa nini ninaona onyo la uwezekano wa kugunduliwa kwa hatari?