Jinsi ya kuripoti biashara au orodha ya katalogi
Ikiwa unahisi kwamba biashara inakiuka Sera yetu ya Biashara, unaweza kuiripoti.
Kuripoti bidhaa au huduma
Ili uripoti bidhaa au huduma:
- Fungua soga na biashara hiyo
- Bofya aikoni ya
iliyo kando ya jina la biashara - Bofya bidhaa au huduma ili uangalie Maelezo.
- Bofya aikoni ya
| > Ripoti bidhaa. - Una chaguo mbili:
- Ili uripoti tu bidhaa au huduma, bofya RIPOTI BIDHAA.
- Ili utoe maelezo zaidi, bofya TUELEZE ZAIDI. Kisha, teua chaguo na ubofye WASILISHA.
Kuripoti biashara
Ili uripoti biashara:
- Nenda kwenye jalada la WhatsApp Business
- Bofya aikoni ya
| kwa chaguo zaidi, inayopatikana katika kona ya juu kulia - Bofya Ripoti biashara.
- Una chaguo mbili:
- Ili uzuie na uripoti biashara, bofya kisanduku cha kuteua kando ya Zuia biashara na ufute ujumbe wa soga hii. Kisha, gusa RIPOTI
- Ili uripoti tu biashara, bofya RIPOTI.