Jinsi ya kusakinisha kiendelezi cha kivinjari cha Code Verify
Kiendelezi cha kivinjari cha Code Verify huongeza safu ya ziada ya usalama kwenye wavuti kwa kuthibitisha kuwa unatumia toleo halisi na lisilobadilishwa la WhatsApp Web. Kiendelezi kinapatikana kwenye vivinjari vifuatavyo:
- Google Chrome
- Mozilla Firefox
- Microsoft Edge
Ili usakinishe kiendelezi cha kivinjari cha Code Verify kwenye kivinjari chako, fuata maagizo yanayotolewa na kivinjari chako. Kwa usaidizi wa ziada, wasiliana na timu ya usaidizi ya kivinjari chako.
Kumbuka:
- Kwa hali bora ya utumiaji, bandika kiendelezi cha Code Verify kwenye upauzana wa kompyuta yako baada ya kupakua ili uweze kuona kiendelezi kwa urahisi na kuthibitisha kama kiliweza kuthibitisha WhatsApp Web.
- Ikiwa unatumia WhatsApp Web kwenye hali fiche au kichupo cha faragha, unapaswa kufuata maagizo ya kivinjari chako ili uruhusu kiendelezi kwenye hali fiche.
- Kiendelezi cha kivinjari cha Code Verify hakitafikia vichupo vya kivinjari chochote au madirisha uliyofungua.
- Kiendelezi hakihifadhi data yoyote, metadata au data ya mtumiaji na hakishiriki taarifa zozote na WhatsApp. Pia hakisomi au kufikia ujumbe unaotuma au kupokea.
Rasilimali zinazohusiana:
- Kuhusu Code Verify
- Kwa nini ninaona hitilafu ya kuisha kwa muda wa mtandao?
- Kwa nini ninaona onyo la kugunduliwa kwa uwezekano wa hatari?
- Kwa nini ninaona onyo la uthibitisho kutofaulu?