Jinsi ya kuingia au kuondoka
Kuingia
Ili uingie kwenye WhatsApp katika WhatsApp Web, WhatsApp Desktop au Portal, unahitaji kutumia simu yako kuchanganua msimbo wa QR.
- Fungua WhatsApp kwenye simu yako.
- Android: Gusa Chaguo zaidi
. - iPhone: Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp.
- Android: Gusa Chaguo zaidi
- Gusa Vifaa Vilivyounganishwa.
- Android: Gusa UNGANISHA KIFAA. Fuata maelekezo kwenye skrini ikiwa kifaa chako kina uthibitishaji wa bayometriki. Ikiwa hujawasha uthibitishaji wa bayometriki, utaombwa uweke PIN ambayo huwa unatumia kufungua simu yako.
- iPhone: Gusa Unganisha Kifaa. Kwenye iOS 14 na matoleo ya baadaye, tumia Touch ID au Face ID kufungua. Ikiwa hujawasha uthibitishaji wa bayometriki, utaombwa uweke PIN ambayo huwa unatumia kufungua simu yako.
- Tumia simu yako kuchanganua msimbo wa QR ulio kwenye kompyuta au Portal yako.
- Ukiulizwa, gusa au chagua Nimemaliza.
Kumbuka: Uthibitishaji hushughulikiwa na mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako kwa kutumia alama za bayometriki zilizohifadhiwa humo. WhatsApp haiwezi kufikia taarifa za bayometriki zilizohifadhiwa kwenye mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako.
Kuondoka
Unaweza kutoka kwenye WhatsApp Web au WhatsApp Desktop kutokea kwenye simu yako, kompyuta au kifaa cha Portal.
Kutoka kwenye kompyuta au Portal yako
- Fungua WhatsApp Web au WhatsApp Desktop.
- Bofya Menyu (
au ) juu ya orodha ya soga zako > Toka.
Kutoka kwenye akaunti ukitumia simu yako
- Fungua WhatsApp kwenye simu yako.
- Android: Gusa Chaguo zaidi
> Vifaa Vilivyounganishwa. - iPhone: Nenda kwenye WhatsApp Mipangilio > gusa Vifaa Vilivyounganishwa.
- Gusa kifaa.
- Gusa TOKA.
Rasilimali zinazohusiana:
- Kuhusu WhatsApp Web na WhatsApp Desktop
- Jinsi ya kupakua WhatsApp Desktop
- Jinsi ya kuongeza au kuondoa akaunti yako ya WhatsApp kwenye Portal
- Imeshindwa kuunganisha WhatsApp