Jinsi ya kuunganisha kifaa
Unaweza kutumia WhatsApp kwenye hadi vifaa vinne vilivyounganishwa kwa wakati mmoja bila ulazima wa simu yako kuwa mtandaoni. Unaweza kuunganisha simu moja tu kwa wakati mmoja.
Kuunganisha kifaa
Fungua WhatsApp Web au WhatsApp Desktop kwenye kifaa unachotaka kukiunganisha.
Android
- Fungua WhatsApp kwenye simu yako.
- Gusa Chaguo zaidi
> Vifaa vilivyounganishwa. - Gusa UNGANISHA KIFAA.
- Fungua simu yako:
- Ikiwa kifaa chako kina uthibitishaji kwa njia ya bayometriki, fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini.
- Ikiwa hujawasha uthibitishaji wa bayometriki, utaombwa uweke PIN ambayo huwa unatumia kufungua simu yako.
- Elekeza simu yako kwenye skrini ya kifaa unachotaka kuunganisha ili uchanganue msimbo wa QR.
iPhone
- Fungua WhatsApp kwenye simu yako.
- Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp.
- Gusa Vifaa Vilivyounganishwa.
- Gusa Unganisha Kifaa.
- Fungua simu yako ikiwa unatumia iOS 14 au matoleo mapya:
- Tumia Touch ID au Face ID ili kufungua.
- Ikiwa hujawasha uthibitishaji wa bayometriki, utaombwa uweke PIN ambayo huwa unatumia kufungua simu yako.
- Elekeza simu yako kwenye skrini ya kifaa unachotaka kuunganisha ili uchanganue msimbo wa QR.
Kumbuka: Kwa hali bora zaidi ya utumiaji, sasisha utumie toleo la hivi karibuni la WhatsApp.