Kuhusu WhatsApp Web na WhatsApp Desktop
Kuna njia mbili za kutumia WhatsApp kwenye kompyuta yako:
- WhatsApp Web: Programu ya WhatsApp inayotegemea kivinjari.
- WhatsApp Desktop: Programu unayoweza kupakua kwenye kompyuta yako.
WhatsApp Web na WhatsApp Desktop ni viendelezi vya kwenye kompyuta vya akaunti yako ya WhatsApp iliyo katika simu yako. Ujumbe unaotuma na kupokea husawazishwa kati ya simu na kompyuta yako na unaweza kuona ujumbe wako kwenye vifaa vyote viwili.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kupakua WhatsApp Desktop
- Jinsi ya kuingia au kutoka
- Imeshindwa kuunganisha WhatsApp Web au WhatsApp Desktop