Jinsi ya kuweka au kuondoa nyota kwenye ujumbe
Kipengele cha jumbe zenye nyota kinakuruhusu kuziwekea alama jumbe maalum ili uweze kuzirejea tena baadaye.
Kuweka nyota kwenye ujumbe
- Vinjari juu ya ujumbe unaotaka kuweka nyota.
- Bofya Menyu
> Weka nyota kwenye ujumbe.
Kumbuka: Kutazama jumbe zako zote zenye nyota, bofya Menyu
Kuondoa nyota kwenye ujumbe
- Vinjari juu ya ujumbe unaotaka kuondoa nyota.
- Bofya Menyu
> Ondoa nyota kwenye ujumbe.
Mbadala:
- Bofya Menyu
au juu ya orodha ya soga > Nyota. - Chagua ujumbe unaotaka kuondoa nyota, ambao utakupeleka kwa ujumbe huo katika soga ya kibinafsi au kikundi.
- Vinjari juu ya ujumbe.
- Bofya Menyu
> Ondoa nyota kwenye ujumbe.
Ondoa nyota kwa jumbe zote
- Bofya Menyu
au juu ya orodha ya soga > Nyota. - Bofya Menyu
au kwa "Jumbe zenye nyota" > Ondoa nyota zote > ONDOA NYOTA.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kuweka au kuondoa nyota kwenye ujumbe: Android | iPhone