Jinsi ya kutuma miitikio ya ujumbe
Unaweza kuitikia ujumbe katika soga zako binafsi na za kikundi ukitumia emoji. Unaweza kuona miitikio yote ya ujumbe kwa kubofya emoji ya miitikio chini ya ujumbe husika.
Kumbuka:
- Unaweza kuweka mwitikio mmoja tu kwa kila ujumbe.
- Miitikio kwenye ujumbe unaotoweka itatoweka wakati ujumbe husika unatoweka.
- Haiwezekani kuficha miitikio au idadi ya miitikio.
- Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe kabla hujauondoa au kama uondoaji haujafanyika. Hutaarifiwa kama uondoaji haukufanyika.
Kuweka mwitikio kwenye ujumbe
Unapoweka mwitikio, ni mtumaji wa ujumbe unaoitikia pekee ndiye atapokea arifa.
- Fanya kiashiria chako kielee juu ya ujumbe, kisha ubofye Menyu > Itikia ujumbe.
- Chagua mojawapo ya emoji zinazoonekana.
Kubadili mwitikio wako
Unaweza kubadilisha mwitikio wako kuwa mwingine.
- Fanya kiashiria chako kielee juu ya ujumbe uliouitikia, kisha bofya Menyu > Itikia ujumbe.
- Chagua emoji tofauti.
Kuondoa mwitiko
Unaweza kuondoa mwitiko wako kwenye ujumbe. Arifa haitatumwa kwa mtumaji wa ujumbe ikiwa utaondoa mwitikio.
- Fanya kiashiria chako kielee juu ya ujumbe uliouitikia, kisha bofya Menyu > Itikia ujumbe.
- Chagua emoji uliyoitika nayo ili uiondoe.