Jinsi ya kutuma maudhui
Kutuma picha, video, nyaraka na anwani
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Bofya Ambatisha
au , kisha bofya: - Picha na Video ili uchague picha au video kutoka kwenye kompyuta yako. Unaweza kutuma hadi picha au video 30 kwa mara moja na kuongeza muktasari kwa kila picha au video. Au, unaweza kuburura na kudondosha picha au video moja kwa moja katika sehemu ya maandishi. Kila video unayotuma haifai kuzidi MB 16.
- Kamera ili upige picha kwa kamera ya kompyuta yako.
- Hati ili uchague nyaraka kutoka kwenye kompyuta yako. Au, unaweza kuburura na kudondosha hati moja kwa moja katika sehemu ya maandishi.
- Anwani ili utume maelezo ya mawasiliano yaliyohifadhiwa kwenye kitabu cha anwani cha simu yako kupitia WhatsApp.
- Bofya Tuma
au .
Kutuma ujumbe wa sauti
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Bofya maikrofoni
au kisha uanze kuzungumza kwenye maikrofoni ya kompyuta yako. - Ukimaliza, bofya Thibitisha
ili utume ujumbe wa sauti.
Kumbuka: Wakati unarekodi ujumbe wa sauti, unaweza kubofya Ghairi
Kuhifadhi picha au video kwenye kompyuta
- Boyfa picha au video unayotaka kuhifadhi.
- Bofya Pakua
au . Ukiulizwa, bofya Hifadhi.