Tuma picha, video, nyaraka, waasiliani au viungo vya Vyumba vya Messenger
Fungua soga ya kibinafsi au kikundi.
Bofya Ambatisha au , kisha bofya:
Picha & Video kuchagua picha au video kutoka kwa kompyuta yako. Unaweza kutuma hadi picha au video 30 kwa mara moja na kuongeza muktasari kwa kila picha au video. Mbadala, unaweza kukokota na kushusha picha au video moja kwa moja kwenye uga wa maandishi. Kuna kikomo cha ukubwa wa MB 16 kwa kila video unayotuma.
Kamera kupiga picha kwa kamera ya kompyuta yako.
Waraka kuchagua nyaraka kutoka kwa kompyuta yako. Mbadala, unaweza kuburuta na kushusha waraka moja kwa moja kwenye uga wa matini.
Mwasiliani kutuma taarifa za waasiliani waliohifadhiwa kwenye kitabu cha anwani cha simu yako kwa WhatsApp.