Jinsi ya kuhakiki ujumbe wa sauti
Kwa kuhakiki rasimu ya sauti uliyorekodi kabla ya kuituma, unaweza kutuma ujumbe wako ukiwa na ujasiri.
Kuhakiki ujumbe wa sauti
Unaweza kusikiliza ujumbe wako wa sauti kabla ya kuutuma.
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Bofya maikrofoni
halafu uanze kuzungumza. - Mara umalizapo, bofya acha
. - Bofya cheza
ili usikilize ulichorekodi. Unaweza pia kubofya sehemu yoyote ya sauti uliyorekodi ili uicheze kutoka hapo. - Bofya debe la taka
ili kufuta ujumbe huo wa sauti, bofya ENDELEA ili uendelee kurekodi, au bofya tuma ili kuutuma.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti