Msimamizi yeyote katika kikundi anaweza kumfanya mshiriki awe msimamizi. Kikundi kinaweza kuwa na idadi isiyo na kikomo ya wasimamizi. Mtu aliyeanzisha kikundi hawezi kuondolewa na atabaki kuwa msimamizi isipokuwa aondoke kwenye kikundi.
Kumfanya mshiriki kuwa msimamizi
Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada.
Au, bofya Menyu ( au ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
Fanya kiashiria kielee juu ya mshiriki unayetaka kumfanya kuwa msimamizi, kisha bofya Menyu.
Bofya Mfanye msimamizi wa kikundi > MFANYE MSIMAMIZI WA KIKUNDI.
Kuwafanya washiriki wengi wasimamizi kwa wakati mmoja
Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada.
Au, bofya Menyu ( au ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
Bofya Mipangilio ya kikundi > Badili wasimamizi wa kikundi.
Chagua washiriki unaotaka kuwafanya wasimamizi.
Bofya alama hakikishi ya kijani unapomaliza.
Kuondoa msimamizi
Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada.
Au, bofya Menyu ( au ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
Fanya kiashiria kielee juu ya msimamizi unayetaka kumwondoa, kisha bofya Menyu.
Bofya Mwondoe kuwa msimamizi.
Kuwaondoa wasimamizi wengi kwa wakati mmoja
Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada.
Au, bofya Menyu ( au ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
Bofya Mipangilio ya kikundi > Badili wasimamizi wa kikundi.
Ondoa alama hakikishi kwenye wasimamizi unaotaka kuwaondoa.