Mtawala yeyote katika kikundi anaweza kumfanya mshiriki mtawala. Kikundi kinaweza kuwa na idadi isiyo na kikomo ya watawala.
Kumbuka: Muumba wa awali wa kikundi hawezi kuondolewa na daima atabaki mtawala isipokuwa aondoke kwenye kikundi.
Kumfanya mshiriki mtawala:
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada.
- Mbadala, bofya Menyu (
au
) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
- Vinjari juu ya mshiriki unayetaka kumfanya mtawala, kisha bofya Menyu
. - Bofya Fanya mtawala wa kikundi > FANYA MTAWALA WA KIKUNDI.
Kumwondoa mtawala:
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada.
- Mbadala, bofya Menyu (
au
) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
- Vinjari juu ya mshiriki unayetaka kumwondoa, kisha bofya Menyu
. - Bofya Ondoa kama mtawala.
Kuwafanya washiriki wengi watawala kwa wakati mmoja:
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada.
- Mbadala, bofya Menyu (
au
) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
- Bofya Mipangilio ya Kikundi > Hariri watawala wa kikundi.
- Chagua washiriki unaotaka kuwafanya watawala.
- Bofya alama hakikishi ya kijani unapomaliza.
Kuwaondoa watawala wengi kwa wakati mmoja:
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada.
- Mbadala, bofya Menyu (
au
) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
- Bofya Mipangilio ya Kikundi > Hariri watawala wa kikundi.
- Usichague watawala unaotaka kuwaondoa.
- Bofya alama hakikishi ya kijani unapomaliza.