Tumia kipengele cha kusambaza ili usambaze ujumbe kutoka kwenye soga ya binafsi au ya kikundi kwenda kwenye soga ya binafsi au ya kikundi. Ujumbe uliosambazwa huashiriwa kwa lebo ya “Ulisambazwa” ili kukusaidia kujua kama rafiki au ndugu yako aliandika ujumbe aliotuma au ikiwa ujumbe huo ulitoka kwa mtu mwingine hapo awali.
Unaposambaza ujumbe unaweza kushirikisha hadi soga tano kwa wakati mmoja. Ujumbe ukiwa umesambazwa mara nyingi, unaweza tu kusambazwa katika soga moja kwa wakati mmoja.
Kumbuka: Ujumbe wowote unaosambaza ambao si wako mwenyewe utaonekana ukiwa na lebo ya "Ulisambazwa" kwako na kwa kila mpokeaji anayepata ujumbe huo.