Jinsi ya kuunda na kualika washiriki kwenye kikundi
Unaweza kuunda kikundi cha WhatsApp chenye hadi washiriki 256.
Kuunda kikundi
- Bofya Menyu (
au ) juu ya orodha yako ya soga kwenye WhatsApp.- Au, bofya aikoni ya Soga mpya.
- Bofya Soga mpya.
- Tafuta au chagua watumiaji unaotaka kuwaweka kwenye kikundi. Kisha bofya aikoni ya kishale cha kijani.
- Weka mada ya kikundi. Hili litakua jina la kikundi ambalo washiriki wote wataliona.
- Ukomo wa mada ni herufi 25.
- Unaweza kuweka emoji kwenye mada yako kwa kubofya aikoni ya Emoji.
- Unaweza kuweka aikoni ya kikundi kwa kubofya WEKA AIKONI YA KIKUNDI
. Unaweza kuchagua Piga picha, Pakua picha au Tafuta kwenye Wavuti ili uweke picha. Ukishaweka, aikoni itaonekana karibu na kikundi kwenye orodha yako ya soga.
- Bofya aikoni ya tiki ya kijani unapomaliza.
Kualika watu kwenye vikundi kupitia viungo
Ukiwa msimamizi wa kikundi, unaweza kuwaalika watu kujiunga na kikundi kwa kushiriki kiungo nao. Msimamizi anaweza Kubadilisha kiungo wakati wowote ili kubatilisha kiungo cha mwaliko wa awali na kuunda kiungo kipya.
- Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bofya mada ya kikundi.
- Au, bofya Menyu (
au ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
- Au, bofya Menyu (
- Bofya Alika kwenye kikundi kwa kutumia kiungo.
- Chagua Tuma kiungo kupitia WhatsApp au Nakili Kiungo.
- Ikiwa unatuma kupitia WhatsApp, tafuta au chagua watu unaowasiliana nao, kisha bofya Tuma.
- Ili kubadilishia kiungo, gusa Weka kiungo upya > WEKA KIUNGO UPYA.
Kumbuka:
- Mtumiaji yeyote wa WhatsApp unayemtumia kiungo cha mwaliko anaweza kujiunga na kikundi, kwa hivyo tumia kipengele hiki tu kwa watu unaowaamini. Inawezekana kwa mtu kusambaza kiungo hicho kwa watu wengine. Ikiwa hivyo, watu hao wengine wanaweza pia kujiunga na kikundi na msimamizi wa kikundi hataulizwa kuwaidhinisha watu hao kabla ya kujiunga.
- Tunaongeza ukubwa wa vikundi hatua kwa hatua katika miezi ijayo na huenda kukawa na kuchelewa kufikia kipengele hiki.