Jinsi ya kutumia hali nyeusi
Hali nyeusi hukuruhusu kubadilisha rangi ya mandhari ya WhatsApp kutoka nyeupe hadi nyeusi.
Tumia hali nyeusi
- Fungua WhatsApp, kisha bofya Menyu
juu ya orodha ya soga zako. - Bofya Mipangilio > Mandhari.
- Chagua miongoni mwa zifuatazo:
- Mwanga: Kuzima hali nyeusi.
- Nyeusi: Kuwasha hali nyeusi.
- Mfumo wa msingi: Kuwasha mandhari meusi ya WhatsApp kulingana na mipangilio ya kifaa chako.