Unaweza kuperuzi mada hapo chini ili kupata kile unachokitafuta.
Jinsi ya kuhariri jalada lako
Kuhariri picha yako ya jalada
Fungua WhatsApp > bofya aikoni ya picha yako ya jalada.
Au, bofya Menyu juu ya orodha ya soga zako > Mipangilio > picha ya jalada lako.
Kama:
Una picha ya jalada: Fanya kiashiri chako kielee juu ya picha yako, kisha bofya BADILISHA PICHA YA JALADA, ambapo unaweza kuchagua Kuangalia picha, Kupiga picha, Kupakia picha, au Kuondoa picha.
Huna picha ya jalada: Bofya WEKA PICHA YA JALADA, ambapo unaweza kuchagua Kupiga picha au Kupakia picha.
Kuhariri jina la jalada lako
Fungua WhatsApp > bofya aikoni ya picha yako ya jalada.
Au, bofya Menyu juu ya orodha ya soga zako > Mipangilio > picha ya jalada lako.
Ili kusasisha jina la jalada lako, bofya Hariri.
Unaweza pia kuweka emoji kwa kubofya Emoji.
Baada ya kumaliza kufanya mabadiliko, bofya alama ya tiki.
Kuhariri taarifa kukuhusu
Fungua WhatsApp > bofya aikoni ya picha yako ya jalada.
Au, bofya Menyu juu ya orodha ya soga zako > Mipangilio > picha ya jalada lako.
Kusasisha maelezo yalio kwenye "kuhusu", bofya Hariri.