Jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi
Katalogi iliyosasishwa huwarahisishia wateja kutangamana na biashara yako. Pia husaidia kuonyesha bidhaa na huduma zako mpya.
Kuweka bidhaa au huduma
Ili uweke bidhaa au huduma kwenye katalogi yako:
- Fungua programu ya WhatsApp Business.
- Bofya Zaidi
| juu ya orodha yako ya soga > Katalogi. - Bofya Ongeza bidhaa mpya.
- Bofya Ongeza Picha ili upakie picha kutoka kwenye faili zako. Unaweza kupakia hadi picha 10.
- Weka jina la bidhaa au huduma. Unaweza pia kuweka taarifa za hiari kama vile bei, maelezo, kiungo na msimbo wa bidhaa unayopakia.
- Gusa ONGEZA KWENYE KATALOGI ili uweke bidhaa kwenye katalogi yako.
Kudhibiti ni bidhaa au huduma zipi wateja wanaweza kuona
Kumbuka: Huenda bado usiweze kutumia kipengele hiki.
Kuficha bidhaa za katalogi
- Fungua programu ya WhatsApp Business.
- Bofya Zaidi
| juu ya orodha yako ya soga > Katalogi. - Bofya bidhaa au huduma unayotaka kuificha > Hariri.
- Chagua Ficha bidhaa.
- Bofya Hifadhi.
Au, fanya kiashiria cha kipanya chako kielee juu ya bidhaa kwenye skrini ya Katalogi. Kisha, bofya Zaidi
Bidhaa zilizofichwa bado zitaonekana kwenye kidhibiti chako cha katalogi zikiwa na
Kufichua bidhaa za katalogi
- Fungua programu ya WhatsApp Business.
- Bofya Zaidi
| juu ya orodha yako ya soga > Katalogi. - Bofya bidhaa au huduma unayotaka kuifichua > Hariri.
- Ondoa uteuzi Ficha bidhaa.
- Bofya Hifadhi.
Au, fanya kiashiria cha kipanya chako kielee juu ya bidhaa kwenye skrini ya Katalogi. Kisha, bofya Zaidi
Kufuta bidhaa au huduma
Ili ufute bidhaa au huduma kutoka kwenye katalogi yako:
- Fungua programu ya WhatsApp Business.
- Bofya Zaidi
| juu ya orodha yako ya soga > Katalogi. - Chagua bidhaa au huduma ambayo ungependa kufuta.
- Sogeza hadi chini kwenye sehemu ya maelezo ya bidhaa.
- Bofya Futa Bidhaa.
- Bofya SAWA.
Kumbuka: Kila picha inayopakiwa kwenye katalogi itakaguliwa. Ukaguzi husaidia kuthibitisha kuwa picha, bidhaa au huduma zinatii Sera za Biashara kwenye WhatsApp.
Ikiwa bidhaa au huduma katika katalogi yako imekataliwa, aikoni nyekundu ya mshangao itaonyeshwa karibu na picha. Ikiwa unahisi hii si sawa na ungependa kuomba ukaguzi mwingine:
- Chagua bidhaa au huduma iliyokataliwa ili uone Maelezo.
- Bofya omba ukaguzi mwingine.
- Bofya PATA MAELEZO ZAIDI ili upitie Sera yetu ya biashara.
- Weka sababu ya ombi katika sehemu ya matini.
- Bofya Endelea.