Kwa sababu ya WhatsApp kutumia picha kutoka Gombo ya Kamera au albamu ya Picha, utahitaji kuipatia programu ruhusa ya kutumia Picha kutoka kwa iPhone yako. Ukikataa kutoa ruhusa kutumia picha, utaona tahadhari hii:
Unaweza kutoa ruhusa kwa kubadilisha mipangilio ya faragha ya simu yako:
Fungua WhatsApp na utaweza kutumia Picha za iPhone ulizonazo sasa kwa WhatsApp.
Hii si suala la kawaida, lakini hutokea kwa idadi ndogo ya watumiaji. Hakikisha kuwa hauna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwenye Mipangilio ya iPhone > Muda wa Skrini. Vinginevyo, bila shaka utahitaji kucheleza na kurejesha simu yako.