WhatsApp inakuruhusu kubinafsisha picha na video zako kwa kuongeza emoji, maandishi, michoro ya mikono na vichujio.
Kumbuka: Vipengele hivi vinapatikana tu kwenye iPhone 5s au mpya na iOS 9 au mpya.
Kuhariri picha na video
- Gusa Ambatisha
karibu na sehemu ya maandishi..
- Piga picha au video mpya, au chagua picha au video iliyopo kutoka kwenye Gombo ya Kamera.
- Anza kuhariri picha yako au video.
Kuongeza emoji
- Gusa Emoji
iliyo juu.
- Chagua emoji.
- Kusogeza emoji, gusa na shikilia, kisha ikokote.
- Kubadilisha ukubwa wa emoji, ifinye na ipanue kuifanya kubwa au ndogo.
- Kuzungusha emoji, finya na ugeuze emoji.
Kuongeza maandishi
- Gusa funguo la "T" hapo juu.
- Andika maandishi yanayotakikana kwenye sehemu ya maandishi.
- Kuchagua rangi, telezesha kidole chako juu na chini kwenye kichaguo cha rangi upande wa kulia.
- Kuchagua aina ya mwandiko, telezesha kidole chako kutoka kwenye kichaguo cha rangi upande wa kulia hadi kushoto. Inua kidole kuthibitisha aina ya mwandiko.
- Kubadilisha ukubwa wa maandishi, yafinye na yapanue kuyafanya makubwa au madogo.
- Kuzungusha maandishi, finya na ugeuze maandishi.
Kuchora
- Gusa Chora
hapo juu.
- Tumia kidole chako ilikuchora michoro.
- Kuchagua rangi, telezesha kidole chako juu na chini kwenye kichaguo cha rangi upande wa kulia. Unaweza kuchagua rangi kwa kila mstari unaouchora.
Kutumia vichujio
- Telezesha juu kwenye picha au video.
- Chagua kichujio.
Kuacha uhariri na kutuma
Kuacha emoji na maandishi, zikokote hadi juu ya skrini kuelekea kwenye takataka na ziachilie. Kufuta michoro, gusa funguo la Tengua. Unapomaliza kuhariri picha zako na video, gusa Tuma
.