Maswali Yanayoulizwa Sana
sw
Chagua lugha yako
  • Azərbaycanca
  • Afrikaans
  • Bahasa Indonesia
  • Bahasa Melayu
  • Català
  • Česky
  • Dansk
  • Deutsch
  • eesti
  • English
  • Español
  • Français
  • Gaeilge
  • Hrvatski
  • Italiano
  • Kiswahili
  • Latviešu
  • Lietuviškai
  • Magyar
  • Nederlands
  • Norsk
  • Oʻzbekcha
  • Pilipino
  • Polski
  • Português (BR)
  • Português (PT)
  • Română
  • shqip
  • Slovenčina
  • Slovenščina
  • suomi
  • svensk
  • Tiếng Việt
  • Türkçe
  • Ελληνικά
  • Български
  • Қазақ
  • Македонски
  • Pусский
  • српски
  • Українська
  • ‏עברית‏
  • العربية
  • فارسی
  • اردو
  • বাংলা
  • हिंदी
  • ગુજરાતી
  • ಕನ್ನಡ
  • मराठी
  • தமிழ்
  • తెలుగు
  • മലയാളം
  • ภาษาไทย
  • 简体中文
  • 繁體中文
  • 日本語
  • 한국어
  • WhatsApp Web
  • Vipengele
  • Pakua
  • Usalama
  • Maswali Yanayoulizwa Sana
  • Pakua
  • Vipengele
  • Usalama
  • Maswali Yanayoulizwa Sana
  • Kuwa karibu

Ni jinsi gani tunaweza kukusaidia?

Unaweza kuperuzi mada hapo chini ili kupata kile unachokitafuta.
AndroidUmezuiliwa kwa Muda

Kuhusu Akaunti Zilizopigwa Marufuku Kwa Muda

Ukipokea ujumbe ndani ya programu unaosema akaunti yako ni "Imepigwa marufuku kwa muda" hii ina maana kwamba huenda unatumia toleo la WhatsApp lisilowezeshwa badala ya programu rasmi ya WhatsApp. Ikiwa haugeuzi ili kutumia programu rasmi baada ya kuzuiliwa kwa muda, akaunti yako inaweza kupigwa marufuku kabisa kutumia WhatsApp.

Programu ambazo haziwezeshwi, kama vile WhatsApp Plus, GB WhatsApp au programu ambazo zinadai kuweza kuhamisha soga zako kati ya simu, ni toleo za WhatsApp zilizobadilishwa. Programu hizi zisizo rasmi hutengenezwa na wengine na kukiuka Masharti ya Huduma yetu. WhatsApp haiwezeshi programu za wahusika wengine kwa sababu hatuwezi kuthibitisha mazoea yao ya usalama.

Jinsi ya kugeuza kwa toleo rasmi ya programu ya WhatsApp

Huenda ukahitaji kucheleza historia yako ya soga kabla ya kuhamia kwa programu rasmi ya WhatsApp. Jina la programu isiyowezeshwa unayotumia huamua kama unahitaji kuhamisha historia yako ya soga. Pata jina la programu kwa kugusa Hiari zaidi > Mipangilio > Msaada > Maelezo ya programu. Fuata hatua zilizopo hapa chini kulingana na jina la programu: WhatsApp Plus au GB WhatsApp.

Ikiwa unatumia programu nyingine isipokua WhatsApp Plus au GB WhatsApp, tunapendekeza hifadhi historia ya soga kabla ya kupakua programu rasmi ya WhatsApp.

GB WhatsApp

Tunapendekeza kufuata hatua zilizopo hapa chini kuhifadhi na kuhamisha historia ya soga yako. Kutofuata hatua hizi kutasababisha kupotea kwa historia ya soga. Tafadhali kumbuka kuwa hatuwezi kuthibitisha hii itakuwa uhamisho wa historia ya mafanikio ya soga kwa sababu WhatsApp haiwezeshi programu zisizo rasmi.

  1. Subiri muda wa kupigwa marufuku uishe. Saa itaonyesha urefu wa kupiga marufuku.
  2. Kwenye GB WhatsApp, gusa Hiari zaidi > Soga > Chelezesha soga.
  3. NendaMipangilio ya Simu > gusa Hifadhi > Faili.
  4. Pata folda ya GB WhatsApp na gusa na shikilia kuichagua.
  5. Katika kona ya juu ya upande wa kulia gusa Zaidi > Badili jina na badili jina la folda kuwa “WhatsApp”.
  6. Nenda kwenye Play Store na upakue programu rasmi ya WhatsApp. Ikiwa huwezi kufikia Play Store, pakua programu hapa.
  7. Kwenye WhatsApp, thibitisha namba ya simu. Jifunze jinsi ya kuthibitisha katika makala hii.
  8. Kwenye skrini ya Chelezo iliyopatikana, gusa Rejesha > Mbele.
  9. WhatsApp inapaswa kupakia na soga zako zilizopo.
WhatsApp Plus

Ikiwa historia yako ya soga ilihifadhiwa awali, inapaswa kuhamisha moja kwa moja kwa programu rasmi ya WhatsApp. Jifunze jinsi ya kuhifadhi historia ya soga yako kwenye Kituo cha Msaada.

  1. Nenda kwenye Play Store na upakue programu ya WhatsApp. Ikiwa huwezi kufikia Play Store, pakua programu hapa.
  2. Thibitisha namba ya simu. Jifunze jinsi ya kuthibitisha katika makala hii.

Rasilimali

  • Ikiwa unatumia toleo rasmi ya programu ya WhatsApp na akaunti yako imepigwa marufuku, rejea makala hii.
  • Jifunze zaidi kuhusu jinsi ya Kutumia WhatsApp kwa wajibu kwenye makala hii.
Makala hii ilikufaidi?
NdiyoLa
Kwanini makala hii haikukufaidi?
  • Makala hii ilikuwa na mkanganyiko
  • Makala hii haikujibu swali langu
  • Suluhisho sio sawa
  • Sipendi kipengele au sera
Asante kwa maoni yako
Mwanzo wa Maswali Yanayoulizwa Sana

WhatsApp

  • Vipengele
  • Usalama
  • Pakua
  • WhatsApp Web
  • Biashara

Shirika

  • Kuhusu
  • Kazi
  • Kituo cha Bidhaa
  • Kuwa karibu
  • Blog
  • Hadithi za WhatsApp

Pakua

  • Mac/PC
  • Android
  • iPhone
  • Windows Phone

Msaada

  • Maswali Yanayoulizwa Sana
  • Twitter
  • Facebook
2019 © WhatsApp Inc.
Faragha na Masharti