Kuunda kikundi
Kuunda kikundi:
- Nenda kwenye tab ya Soga kwenye WhatsApp.
- Chagua kikundi kipya
.
- Watafute au chagua waasiliani wa kuongeza kwenye kikundi. Kisha gusa ikoni ya angalia
.
- Ingiza mada ya kikundi. Hii itakuwa jina la kikundi ambacho washiriki wote wataliona.
- Kikomo cha mada ni herufi 25.
- Unaweza kuongeza emoji kwenye mada kwa kubofya ikoni ya emoji.
- Kwa hiari, ongeza ikoni ya kikundi kwa kugusa ongeza picha, ambapo unaweza kufanya yafuatayo chukua picha
, chagua kutoka kwa albamu au tafuta tovuti kupata picha. Ukishaweka, ikoni itaonekana karibu na kikundi kwenye tab ya Soga.
- Gusa unda
unapomaliza.
Kualika kwa vikundi kwa kupitia viungo
Ukiwa mtawala wa kikundi, unaweza kuwaalika watu kujiunga na kikundi kwa urahisi kwa kushirikisha kiungo nao. Kushirikisha kiungo cha mwaliko wa kikundi:
- Nenda kwenye kikundi kwa WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Mbadala, bonyeza kwa muda kikundi kwenye tab ya Soga. Kisha gusa maelezo ya kikundi.
- Gusa ongeza mshiriki (+) > alika kwenye kikundi kwa kupitia kiungo.
- Chagua tuma kiungo kupitia WhatsApp, nakili kiungo au shirikisha kiungo tumia programu nyingine.
- Mtawala anaweza kutangua kiungo wakati wowote kufanya kiungo cha awali cha mwaliko batiki na kuunda kiungo kipya.
Kumbuka: Mtumiaji yeyote wa WhatsApp unayemshirikisha kiungo cha mwaliko anaweza kujiunga na kikundi, kwa hivyo tumia kipengele hiki tu na watu wanaoaminika. Inawezekana kwa mtu kusambaza kiungo kwa watu wengine. Ikiwa hivyo, watu hao wengine wanaweza pia kujiunga na kikundi na mtawala wa kikundi hataulizwa kuwaidhinisha watu hao kabla ya kujiunga.
Jifunze jinsi ya kuunda na kualika kwa vikundi kwenye: Android | iPhone | WhatsApp Web