Kipengele cha Bofya kupiga Soga cha WhatsApp kinakuruhusu kuanzisha soga na mtu bila ya namba ya simu yao ya simu kuhifadhiwa kwenye kitabu chako cha anwani cha simu yako. Iloimradi unajua namba ya simu ya mtu huyu, unaweza kuunda kiungo kinachokuwezesha kuanza kuupiga soga naye. Kwa kubofya kiungo, soga na mtu huyo inafunguka kiotomatiki. Bofya kupiga Soga hufanya kazi kwa simu yako na WhatsApp Web.
Kuunda kiungo chako, tumia https://wa.me/<number>
ambapo <number>
ni namba ya simu kamili katika muundo kwa kimataifa. Acha sufuri zozote, mabano au vistari wakati wa kuongeza namba ya simu katika muundo wa kimataifa. Kwa maelezo zaidi kuhusu namba za kimataifa, soma makala hii. Tafadhali kumbuka kwamba namba hii ya simu lazima iwe na akaunti inayofanya kazi kwenye WhatsApp.
Tumia: https://wa.me/15551234567
Usitumie: https://wa.me/+001-(555)1234567
Kuunda kiungo chako kilichojazwa na ujumbe utaonekana kiotomatiki kwenye sehemu ya maandishi ya soga, tumia https://wa.me/whatsappphonenumber/?text=urlencodedtext
ambapo whatsappphonenumber
ni namba ya simu iliyo kwenye muundo wa kimataifa kamilifu URL-encodedtext
ni usimbaji wa URL uliojazwa na ujumbe.
Mfano:https://wa.me/15551234567?text=I'm%20interested%20in%20your%20car%20for%20sale
Kuunda kiungo chako kilichojazwa na ujumbe, tumia https://wa.me/?text=urlencodedtext
Mfano:https://wa.me/?text=I'm%20inquiring%20about%20the%20apartment%20listing
Baada ya kubofya kiungo, utaonyeshwa orodha ya waasiliani unaoweza kuwatumia ujumbe.