Tunajali kuhusu faragha yako. Jumbe na simu zote za WhatsApp zimelindwa kwa ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho. Hii inahakikisha kuwa wewe tu na mtu unayewasiliana naye mnaweza kusoma au kusikiliza simu zako, na hakuna mtu katikati, hata WhatsApp.
Kwa hali zote, WhatsApp itatuma jumbe zako kwa biashara zikiwa zimefumbwa mwisho-kwa-mwisho. Ni muhimu kukumbuka, hata hivyo, kuwa unapowasiliana na biashara, watu wengi katika biashara hiyo wanaweza kuona jumbe zako. Aidha, baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia huduma zetu za WhatsApp Business wanaweza kutumia kampuni nyingine kusimamia mawasiliano yao - kwa mfano, kuhifadhi, kusoma au kujibu jumbe zako.
Biashara unayowasiliana nayo ina jukumu la kuhakikisha kwamba inashughulikia ujumbe wako kwa mujibu wa sera yake ya faragha. Kwa habari zaidi, tafadhali wasiliana na biashara hiyo moja kwa moja.
Kwa habari zaidi kuhusu mpango wetu wa ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho, tafadhali soma nakala hii.