Kwa jibu za haraka, unaweza kuunda njiamkato ya kiandikio kwa jumbe unazotuma mara nyingi. Unaweza kutumia maandishi au emoji kwenye majibu ya haraka.
Kuweka jibu za haraka:
- Gusa Mipangilio > Zana za Biashara > Ujumbe wa haraka.
- Gusa kwenye ikoni ya jumlisha (+) iliyopo kwenye kona ya juu upande wa kulia ili kuunda jibu jipya la haraka.
- Chini ya Ujumbe, gusa kuandika ujumbe wa jibu la haraka.
- Gusa /Njiamkato kuandika njiamkato ya kiandikio kwa jibu la haraka.
Weka nenomsingi ili lipatikane upesi.
Dondoo: Maneno msingi ni muhimu katika kuchangua kama una majibu mengi ya haraka yaliyohifadhiwa kwenye orodha yako. Unaweza kuongeza mpaka maneno msingi matatu kwa kila jibu la haraka.
- Gusa Hifadhi.
Kutumia majibu ya haraka:
- Fungua soga.
- Kwenye uga la ingizo la maandishi, andika “/” iki fuatiliwa na njiamkato ya jibu la haraka lililowekwa awali.
- Chagua jibu la haraka. Kiolezo cha ujumbe kitaweka kiotomatiki kwenye uga ya ingizo ya maandishi.
- Unaweza kuhariri jumbe au kugusa tu Tuma.
Kuchangua majibu ya haraka
Ikiwa una majibu mengi ya haraka, unaweza kuchangua kupitia orodha yako ya maneno msingi na matumizi. Maneno msingi ya majibu ya haraka yanayoonekana kwenye mazungumzo sasa yanaonyeshwa kwanza, ikifuatiwa na majibu ya haraka yaliyotumiwa hivi karibuni. Kwa mfano: Ukiwa na jibu la haraka lililohifadhiwa kimaalum kila mwezi, unaweza kuongeza maneno msingi kama vile "maalum" na "kila mwezi" kwa jibu la haraka. Sasa, wakati ujumbe wa mteja una mojawapo ya maneno hayo, jibu la haraka litawekwa juu. Ikiwa majibu mengine ya haraka yanalingana na maneno msingi, yatapangwa kwa kialfabeti.
Kwa nini siwezi kuhifadhi jibu langu la haraka?
Kuna vikwazo fulani vya kukumbuka wakati wa kuhifadhi majibu yako ya haraka. Haya ni pamoja na:
- Idadi ya juu inayokubaliwa ya kuhifadhi majibu ya haraka ni 50.
- Urefu wa juu wa njia-mkato ya jibu la haraka ni herufi 25.
- Nafasi za kuongoza na kufuatilia kutoka kwa njia ya mkato zinaondolewa.
- Njiamkato zote lazima zianze na mkwaju mbele '/'.
- Idadi ya juu ya maneno msingi yanayoruhusiwa kwa kila jibu la haraka ni 3.
- Maneno msingi yasiwe na nafasi au herufi zozote zifuatazo: '!', '#', '$', '%', '&', '(', ')', '*', '+', '-', '.', '/', '\', ':', ';', '<', '=', '>', '?', '@', '[', ']', '^', '_', '`', '{', '|', '}', '~', '×', '÷', '"'.
- Kikomo cha urefu wa neno moja la msingi ni herufi 15.
Dondoo: Emoji zinaweza kutumika katika njiamkato na majibu ya haraka.