Kushiriki viungo vya katalogi
Katalogi inawaruhusu wateja wa sasa na wanaotarajiwa kuvinjari bidhaa au huduma za biashara na kuuliza maswali na kuwasiliana na biashara. Wateja wanaweza kuchagua bidhaa au huduma wanayovutiwa nayo, na kuishiriki kwa marafiki zao au kutuma ujumbe kwa biashara ili kuuliza maswali kuhusu bidhaa.
Kushiriki bidhaa au huduma kutoka kwa katalogi:
- Nenda kwa Katalogi
- Chagua kitu au huduma unayopenda kushiriki
- Gusa kwenye nukta tatu zilizopo kwenye kona ya juu kulia
- Kisha unaweza kushiriki kitu maalumu kwenye katalogi yako na waasiliani wako au wanunuzi tarajiwa popote pale kwa kuchagua hiari yoyote:
- Mbele: kushiriki kiungo cha vitu na wengine kwenye WhatsApp.
- Shiriki: kushiriki kiungo cha kitu kwa barua pepe au programu za utumaji ujumbe za mhusika mwingine.
- Chagua soga za vikundi au kibinafsi unazotaka kushiriki kitu au huduma nazo.
- Gusa Tuma
Kushiriki kiungo kutafungua moja kwa moja vitu/katalogi kama mpokeaji atatazama kiungo kwenye WhatsApp Messenger au programu ya WatsApp Business.
Hata hivyo, kama kiungo cha katalogi kimeshirikishwa kwa barua pepe au kivinjari, kiteuzi kiItafunguka kuruhusu mtumiaji kuchagua programu ipi ifungue kiungo.