Jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi
Katalogi iliyosasishwa huwarahisishia wateja kutangamana na biashara yako. Pia husaidia kuonyesha bidhaa na huduma zako mpya.
Kuongeza bidhaa au huduma kwenye katalogi yako
- Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
- Ikiwa unaunda katalogi mpya, gusa Ongeza Bidhaa au Huduma.
- Gusa aikoni ya buluu ya jumlisha au Ongeza bidhaa mpya. Kisha, gusa Ongeza Picha.
- Gusa Chagua Picha ili upakie picha kutoka kwenye Picha au Piga Picha ili upige picha mpya. Unaweza kupakia hadi picha 10.
- Weka jina la bidhaa au huduma. Pia unaweza kuweka taarifa za hiari kama vile bei, maelezo, kiungo cha tovuti na msimbo wa bidhaa au huduma kwa ajili ya bidhaa unayopakia.
- Gusa Hifadhi.
Kudhibiti bidhaa au huduma ambazo wateja wanaweza kuona
Kumbuka: Huenda bado usiweze kutumia kipengele hiki.
Kuficha bidhaa za katalogi
- Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
- Gusa bidhaa au huduma unazotaka kuficha > Zaidi
> Hariri. - Washa Ficha bidhaa hii.
- Gusa Hifadhi.
Au, telezesha kushoto kwenye bidhaa iliyo katika kidhibiti cha Katalogi. Kisha, gusa Ficha > Ficha.
Bidhaa ulizoficha bado zitaonekana kwenye kidhibiti chako cha katalogi zikiwa na
Kufichua bidhaa za katalogi
- Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
- Gusa bidhaa au huduma unayotaka kuifichua > Zaidi
> Hariri. - Zima Ficha bidhaa hii.
- Gusa Hifadhi.
Au, telezesha kushoto kwenye bidhaa iliyo katika kidhibiti cha Katalogi. Kisha, gusa Fichua > Fichua.
Futa bidhaa au huduma kutoka kwenye katalogi yako
- Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
- Telezesha kushoto kwenye bidhaa au huduma unayopenda kufuta. Kisha, gusa Futa > Futa.
Au, chagua picha ya bidhaa au huduma unayotaka kuifuta. Kisha, gusa Hariri > Futa > Futa.
Kumbuka: Kila picha inayopakiwa kwenye katalogi itakaguliwa. Ukaguzi husaidia kuthibitisha kuwa picha, bidhaa au huduma zinakidhi Sera za Biashara za WhatsApp.