Programu ya WhatsApp Business ni programu iliyo bure kupakua kwa biashara ndogo.
Kabla ya kupakua programu, tafadhali fahamu yafuatayo:
Ikiwa una akaunti ya WhatsApp Messenger, unaweza kwa urahisi kuhamisha akaunti yako, pamoja na historia ya soga na media, kwa akaunti mpya ya WhatsApp Business.
Historia yako ya soga haiwezi kurudishwa kwa WhatsApp Messenger kama ukiamua kuacha kutumia programu ya WhatsApp Business.
Unaweza kutumia programu ya WhatsApp Business na pia WhatsApp Messenger wakati huo huo ilimradi akaunti zimeunganishwa na namba tofauti za simu. Haiwezekani kuwa na namba moja ya simu inayotumia programu zote mbili kwa wakati mmoja.