Unaweza kutuma ujumbe wa salamu kiotomatiki kwa wateja wanapokutumia ujumbe mara ya kwanza au baada ya siku 14 za kutokuwa na soga nawe.
Kuweka ujumbe wa salamu:
- Gusa Hiari zaidi
> Zana za Biashara > Ujumbe wa salamu. - Washa Tuma ujumbe wa salamu.
- Hariri ujumbe kwa kuugusa.
- Chini ya Wapokeaji, gusa na uchague kati ya:
- Kila mtu ili utume ujumbe wa salamu kwa kila mtu anayekutumia ujumbe baada ya saa za biashara.
- Kila mtu asiye kwenye kitabu cha anwani ili utume ujumbe wa salamu kwa nambari ambazo hazipo kwenye kitabu chako cha anwani.
- Kila mtu isipokuwa... ili utume ujumbe wa salamu kwa nambari zote isipokuwa chache unazochagua.
- Tuma tu kwa... ili utume ujumbe wa salamu kwa wapokeaji unaowachagua.
- Gusa HIFADHI.
Kumbuka: Ujumbe wa salamu hutumwa tu wakati simu yako ina muunganisho wa intaneti unayofanya kazi.