Ukiwa na shughuli nyingi au haupo ofisi, unaweza kuweka ujumbe unaotumwa kiotomatiki kwa waasiliani wako wote au baadhi yao kwamba haupo. Unaweza pia kupanga ratiba ya ujumbe wa kuwa mbali ili kuwasha kiotomatiki wakati fulani, kwa mfano, wakati biashara yako imefungwa.
Kuweka ujumbe wa kutokuwepo:
Gusa Chaguo zaidi > Zana za biashara > Ujumbe wa kutokuwepo.
Washa Tuma ujumbe wa kutokuwepo.
Gusa ujumbe ili kuuhariri > SAWA.
Chini ya Ratibu, gusa na uchague kati ya:
Tuma kila wakati ili utume ujumbe wa kiotomatiki kila wakati.
Ratiba maalum ili utume ujumbe kiotomatiki wakati maalum tu.
Nje ya saa za biashara ili utume ujumbe wa kiotomatiki nje ya saa za biashara tu. Chaguo hili linapatikana tu kama umeweka saa zako za biashara kwenye jalada lako la biashara. Pata maelezo ya jinsi kufanya hivyo kwenye makala haya.
Chini ya Wapokeaji, gusa na uchague kati ya:
Kila mtu ili utume ujumbe wa kiotomatiki kwa yeyote anayekutumia ujumbe nje ya saa za biashara.
Kila mtu asiye kwenye kitabu cha anwani ili utume ujumbe wa kiotomatiki kwa nambari ambazo hazipo kwenye kitabu chako cha anwani.
Kila mtu isipokua... ili utume ujumbe wa kiotomatiki kwa kila nambari isipokuwa chache unazochagua.
Tuma tu kwa... ili utume ujumbe wa kiotomatiki kwa waasiliani unaowachagua.
Gusa Hifadhi.
Kumbuka: Ujumbe wa kutokuwepo hutumwa tu wakati simu yako ina muunganisho wa intaneti unaofanya kazi.