Unaweza kushiriki bidhaa na huduma zako na wateja wapya na waliopo kwa kushiriki katalogi yako.
Shiriki katalogi yako kwenye soga ya kibinafsi au soga ya kikundi
- Fungua soga kwenye programu ya WhatsApp Business.
- Gusa aikoni ya kiambatisho karibu na uga wa maandishi.
- Kisha, gusa Katalogi.
- Gusa Tuma vitu vyote hapo juu.
Shiriki bidhaa au huduma kwenye soga ya kibinafsi au soga ya kikundi
- Fungua soga kwenye programu ya WhatsApp Business.
- Gusa aikoni ya kiambatisho karibu na uga wa maandishi.
- Kisha, gusa Katalogi.
- Teua bidhaa au huduma unayo taka shiriki.
- Gusa Tuma.
Shiriki katalogi yote kupitia kwa Kisimamizi cha Katalogi
- Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
- Mara unapokuwa kwenye Kisimamizi cha Katalogi, gusa aikoni ya kiungo kilichopo juu upande wa kulia.
- Kisha unaweza kushiriki katalogi nzima na waasiliani wako au wanunuzi tarajiwa popote kwa kuchagua hiari yoyote:
- Tuma kiungo kupitia WhatsApp Business: kushiriki kiungo cha katalogi na wengine kwa WhatsApp
- Nakili Kiungo: kunakili kiungo
- Shiriki Kiungo: kushiriki katalogi kupitia barua pepe au programu zingine za utumaji ujumbe.
Shiriki bidhaa au huduma binafsi kupitia Kisimamizi cha Katalogi
- Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
- Kutoka kwa Kisimamizi cha Katalogi, chagua vitu unavyotaka kushiriki. Kisha, gusa aikoni ya kiungo iliyopo juu upande wa kulia.
- Unaweza kushiriki kitu maalumu kwenye katalogi yako na waasiliani wako au wanunuzi tarajiwa popote pale kwa kuchagua hiari yoyote:
- Tuma kiungo kupitia WhatsApp Business: kushiriki viungo vya vitu vilivyoteuliwa na wengine kupitia WhatsApp
- Nakili Kiungo: kunakili kiungo
- Shiriki Kiungo: kushiriki kitu kilichochaguliwa kwa njia ya barua pepe au vituo vya jamii.
Katalogi na viungo vya vitu haviwezi kubinafsishwa kabla ya kushirikishwa kwani vinatolewa kiotomatiki.