Jinsi ya kuhariri jalada lako la biashara
Jalada lako la biashara linakuruhusu kuongeza maelezo kuhusu kampuni yako, ikiwa ni pamoja na jina la biashara yako, anwani, aina, maelezo, anwani ya barua pepe na tovuti. Watu wanaweza kuona maelezo haya kwa urahisi wanapoangalia jalada lako.
Ili uangalie jalada la biashara yako, fungua programu ya WhatsApp Business. Kisha, gusa Chaguo zaidi
Kuhariri picha yako ya jalada
- Gusa Hariri
kwenye picha yako ya jalada. - Gusa Matunzio ili kuchagua picha iliyopo au Kamera ili kupiga picha mpya. Unaweza pia kugusa Ondoa picha ili kuondoa picha yako iliyopo.
- Baada ya kuchagua picha au kupiga mpya, punguza au zungusha picha unavyotaka.
- Gusa Nimemaliza.
Kuhariri jina na maelezo ya biashara yako
- Gusa Hariri
kwenye eneo unalotaka kusasisha. - Fanya masasisho yako.
- Gusa SAWA au HIFADHI.
Kuhariri aina ya biashara yako
- Gusa Hariri
katika sehemu ya aina. - Chagua hadi aina tatu zinazofaa kwa ajili ya biashara yako.
Kuhariri anwani ya biashara yako
- Gusa Hariri
katika sehemu ya anwani. - Gusa sehemu ya Anwani > weka anwani ya biashara yako.
- Unaweza pia kusasisha ramani ya mahali pako kwa kugusa WEKA MAHALI KWENYE RAMANI au SASISHA MAHALI KWENYE RAMANI.
- Kisha, sasisha anwani ya biashara yako kwenye ramani au chagua mojawapo ya zifuatazo:
- SASISHA ili ramani ionyeshe ulichoweka katika sehemu ya anwani.
- HARIRI ANWANI ili kurudi katika sehemu ya anwani ya biashara halafu ubadilishe anwani yako.
- ACHA NIWEKE MAHALI ili kutafuta mahali maalumu kwenye ramani.
- Gusa NIMEMALIZA. Kumbuka: Kufanya hivi kunabadilisha tu eneo la biashara yako kwenye ramani. Anwani uliyoweka katika sehemu ya anwani itabaki ilivyo.
- Gusa HIFADHI.
Kuhariri saa za kazi za biashara yako
- Gusa Hariri
katika sehemu ya saa za kazi. - Gusa Ratiba.
- Chagua mojawapo ya vielelezo vya ratiba vifuatavyo:
- Imefunguliwa kwa saa maalumu: Tumia kitufe cha kugeuza ili kuchagua siku maalumu ambazo huwa unafungua. Unaweza pia kuonyesha vikundi vya saa maalumu za kazi kwa kila siku.
- Imefunguliwa kila wakati: Tumia kitufe cha kugeuza ili kuchagua ni siku zipi za juma biashara yako imefunguliwa.
- Kwa miadi tu: Tumia kitufe cha kugeuza ili kuchagua siku ipi ya juma biashara yako ipo wazi kupokea miadi.
- Gusa Hifadhi.
Unaweza pia kugusa Chaguo zaidi > Futa ili kuweka upya saa zako za kazi.
Kuhariri anwani yako ya barua pepe na tovuti
- Gusa Hariri
katika sehemu unayotaka kusasisha. - Kusasisha taarifa zako.
- Gusa HIFADHI.
Kuhariri katalogi yako
- Gusa DHIBITI ili kusasisha katalogi yako au kuunda nyingine mpya.
- Ongeza au hariri vitu kwenye katalogi yako unavyotaka. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi kwenye makala haya.
Kuhariri taarifa zilizo katika sehemu ya "Kukuhusu"
- Gusa Hariri
katika sehemu ya Kuhusu. - Unaweza kuunda ujumbe maalumu wa Kuhusu au kuchagua moja ya zilizowekwa awali kwenye sehemu ya Chagua Kuhusu.
Kuhariri nambari yako ya simu
Gusa Hariri
Rasilimali zinazohusiana:
- Kuhusu jalada lako la biashara
- Jinsi ya kuhariri jalada lako la biashara: iPhone | Web na Desktop