Jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi
Katalogi iliyosasishwa hufanya kuwa rahisi kwa wateja wako kuingiliana na biashara yako. Pia husaidia kuonyesha bidhaa na huduma zako mpya.
Kuongeza bidhaa au huduma kwenye katalogi yako
- Fungua programu ya WhatsApp Business > Chaguo zaidi
> Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi. - Ikiwa unaunda katalogi mpya, gusa Ongeza bidhaa mpya.
- Gusa aikoni ya jumlisha, kisha Ongeza Picha.
- Gusa Matunzio ili upakie picha kutoka kwenye Picha zako au Kamera ili upige picha mpya. Unaweza kupakia hadi picha 10.
- Toa jina la bidhaa au huduma. Unaweza pia kutoa maelezo ya hiari kama vile bei, maelezo, kiungo cha tovuti na bidhaa au msimbo wa huduma ya bidhaa iliyopakiwa.
- Gusa HIFADHI.
Kudhibiti ni bidhaa au huduma zipi wateja wanaweza kuona
Kumbuka: Huenda bado usiweze kutumia kipengele hiki.
Kuficha bidhaa za katalogi
- Fungua programu ya WhatsApp Business > Chaguo zaidi
> Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi. - Unaweza kuficha kitu kimojakimoja au vingi kwa pamoja.
- Ili ufiche kitu kimoja, kiguse ili ufungue ukurasa wa maelezo ya bidhaa hiyo. Kisha, gusa Chaguo zaidi
> Ficha > FICHA. - Ili ufiche vitu kwa pamoja, bonyeza na ushikilie mojawapo ya vitu unayotaka kuficha mpaka alama ya kijani ionekane. Kisha, gusa vitu vingine unavyotaka kuficha > Ficha
> FICHA.
Bidhaa ulizoficha bado zitaonekana kwenye kidhibiti chako cha katalogi zikiwa na
Kufichua bidhaa za katalogi
- Fungua programu ya WhatsApp Business > Chaguo zaidi
> Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi. - Unaweza kufichua kitu kimojakimoja au vingi kwa pamoja.
- Ili ufichue kitu kimoja, kiguse ili ufungue ukurasa wa maelezo ya bidhaa hiyo. Kisha, gusa Chaguo zaidi
> Fichua > FICHUA. - Ili ufichue vitu kwa pamoja, bonyeza na ushikilie mojawapo ya vitu unayotaka kuficha mpaka alama ya kijani ionekane. Kisha, gusa bidhaa unayotaka kufichua > Fichua
> FICHUA.
Kufuta bidhaa au huduma kutoka kwenye katalogi yako
- Fungua programu ya WhatsApp Business > gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio> Zana za Biashara > Katalogi. - Bonyeza na ushikilie picha ya bidhaa au huduma unayotaka kufuta.
- Gusa aikoni ya Futa, kisha gusa NDIYO.
Mbadala, chagua picha ya bidhaa au huduma unayotaka kuifuta. Kisha, gusa Chaguo zaidi
Kumbuka:
- Kila picha inayopakiwa kwenye katalogi itakaguliwa. Ukaguzi unasaidia kuthibitisha kuwa picha, bidhaa au huduma zinakidhi Sera za Biashara ya WhatsApp.
- Ikiwa akaunti yako ya WhatsApp Business imeunganishwa na duka la Facebook na umewasha WhatsApp kuwa kituo cha mauzo, nafasi ya katalogi yako ya WhatsApp huchukuliwa na duka lako la Facebook kwa kawaida. Hatua hii haitafuta au kubadilisha katalogi yako ya WhatsApp, lakini wewe na wateja wako hamtaiona. Unaweza kurudi kwenye katalogi yako ya WhatsApp wakati wowote kwa kuzima au kuficha WhatsApp isiwe kituo cha mauzo. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti kituo chako cha mauzo kwenye Kidhibiti cha Biashara katika makala haya.