Ikiwa unatumia programu ya WhatsApp Business, unaweza kushiriki kiungo kifupi na wateja wako ili waweze kukitumia kuanzisha soga na wewe.
Kuunda kiungo kifupi
Kiungo kifupi cha biashara yako huundwa kiotomatiki unapounda akaunti kwenye programu ya WhatsApp Business. Kufikia kiungo hiki kifupi:
- Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za biashara.
- Gusa Kiungo kifupi kutazama kiungo kilichoundwa kiotomatiki.
Mara unapokifikia kiungo kifupi, unaweza:
- Kugusa
ikiwa unataka kunakili kiungo kifupi na kukibandika kwingine kwenye tovuti yako au kwenye kurasa zingine za Facebook. - Kugusa
kama unataka kutuma kiungo moja kwa moja kwa wateja wako. Mtu yeyote ambaye ana ufikiaji wa kiungo anaweza kukutumia ujumbe. - Kugusa kitelezi ili kuweka kiolezo cha ujumbe kwa wateja kutumia wanapofungua kiungo kifupi.
- Kugusa
ili kuunda na kuhariri ujumbe wako wa kawaida.
Dokezo: Wateja wako wataweza kuhariri ujumbe wa chaguo-msingi.
Rasilimali zinazohusiana
Kuhusu kiungo kifupi kwenye iPhone