Hadhi inakuruhusu kushirikisha sasisho za maandishi, picha, video na GIF zinazopotea baada ya masaa 24. Ili kutuma na kupokea sasisho za hadhi kutoka kwa waasiliani wako, wote wewe na waasiliani wako lazima muwe na namba za simu za kila mmoja wenu zilizohifadhiwa katika vitabu vyenu vya anwani.
Kutazama au kujibu sasisho ya hadhi
- Kutazama sasisho ya hadhi ya mwasiliani, gusa Hadhi
, kisha hadhi ya mwasiliani.
- Kujibu sasisho ya hadhi ya mwasiliani, gusa Jibu
unapotazama.
Kuunda na kutuma sasisho ya hadhi
- Gusa Hadhi
.
- Gusa:
- Kamera
au Hadhi yangu kuchukua picha, rekodi video au GIF au chagua picha, video au GIF uliyonayo kutoka kwa sanaa. Unaweza pia kuongeza muktasari au kuhariri picha, video au GIF, ambavyo unaweza kujifunza jinsi ya kufanya kwenye makala hii.
- Maandishi
kuandika sasisho ya hadhi. Unaweza kugusa T kuchagua mwandiko au Rangi
kuchagua rangi ya mandharinyuma.
- Gusa Tuma
.
Mbadala, unaweza kuunda na kutuma sasisho ya hadhi ya picha, video au GIF kwa kugusa Kamera
.
Kufuta sasisho ya hadhi yako
- Gusa Hadhi
.
- Gus Hadhi Yangu.
- Una hiari kadhaa:
- Gusa Zaidi
karibu na sasisho ya hadhi unayotaka kufuta. Kisha gusa Futa
> Futa Sasisho ya Hadhi 1.
- Telezesha kushoto sasisho ya hadhi unayotaka kufuta, kisha gusa Futa > Futa.
- Ikiwa unataka kufuta sasisho nyingi za hadhi, gusa Hariri. Chagua sasisho za hadhi unazotaka kufuta, kisha gusa Futa > Futa Sasisho za Hadhi {nambari}.
Kusambaza sasisho ya hadhi yako
- Gusa Hadhi
.
- Gus Hadhi Yangu.
- Una hiari mbili:
- Gusa Zaidi
karibu na sasisho ya hadhi unayotaka kusambaza, kisha gusa Sambaza
.
- Ikiwa unataka kusambaza sasisho nyingi za hadhi, gusa Hariri. Chagua sasisho ya hadhi unayotaka kusambaza, kisha gusa Sambaza.
- Tafuta au chagua soga za kibinafsi au vikundi unazotaka kusambazia ujumbe.
- Gusa Sambaza.
Kutuliza na kuliza sasisho ya hadhi ya mwasiliani
Kutuliza sasisho ya hadhi ya mwasiliani
Unaweza kutuliza sasisho ya hadhi ya mwasiliani fulani ili wasionekane juu ya tab ya Hadhi
tena.
- Gusa Hadhi
.
- Telezesha kushoto sasisho ya hadhi ya mwasiliani wako.
- Gusa Tuliza > Tuliza.
Kuliza sasisho ya hadhi ya mwasiliani
- Gusa Hadhi
.
- Sogeza chini kwa sehemu ya SASISHO ZILIZOTULIZWA.
- Telezesha kushoto sasisho ya hadhi ya mwasiliani wako.
- Gusa Liza > Liza.
Rasilimali
- Jifunze jinsi ya kushirikisha Hadhi ya WhatsApp kwa programu zingine kwenye makala hii.
- Jifunze zaidi kuhusu faragha ya hadhi kwenye makala hii.
- Jifunze jinsi ya kutumia Hadhi kwenye: Android