Kwa kipengele cha Orodha ya Tangazo unaweza kutuma ujumbe kwa waasiliani kadhaa kwa mara moja.
Orodha za Tangazo ni orodha zilizohifadhiwa za wapokeaji wa ujumbe ambao unaweza kuwatumia mara kwa mara orodha za jumbe, bila kuwachagua kila mara.
Kuunda Orodha ya Tangazo:
Hii itaunda orodha mpya ya wapokeaji wa tangazo. Unapotuma ujumbe kwa Orodha ya Tangazo, itatuma kwa wapokeaji wote kwenye orodha. Wapokeaji watapokea ujumbe kama ujumbe wa kawaida. Wakijibu, itaonekana kama ujumbe wa kawaida kwenye skrini yako ya Soga; na jibu lao halitatumwa kwa wapokeaji wengine kwenye Orodha ya Tangazo.
Kumbuka: Waasiliani tu waliokuongeza kwenye kitabu cha anwani cha simu zao watapokea ujumbe wako wa tangazo. Ikiwa mwasiliani wako hapokei jumbe za mangazo yako, angalia kuhakikisha kuwa wamekuongeza kwenye vitabu vyao vya anwani. Orodha za Tangazo ni mawasiliano ya moja-kwa-wengi. Ukitaka wapokeaji washiriki kwenye mazungumzo ya kikundi, unapaswa kuunda Soga ya Kikundi badala yake.
Jifunze zaidi kuhusu kutumia Orodha ya Tangazo kwenye: iPhone | Windows Phone