Hatuwezeshi vifaa ambavyo vimefunguliwa kinyume cha sheria na WhatsApp haitafanya kazi kikamilifu kama simu yako imefunguliwa kinyume cha sheria. Ukitaka kutumia WhatsApp na simu yako imefunguliwa kinyume cha sheria, unapaswa kurejesha iPhone yako kwa mipangilio ya kiwanda. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurejesha, zuru tovuti ya Msaada wa Apple.
Kumbuka: Vifaa vilivyofunguliwa kinyume cha sheria haviruhusu muundo wa usalama wa WhatsApp kufanya kazi kama ilivyopangwa na jumbe zako hazitalindwa na ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho.