Maswali Yanayoulizwa Sana
sw
Chagua lugha yako
  • Azərbaycanca
  • Afrikaans
  • Bahasa Indonesia
  • Bahasa Melayu
  • Català
  • Česky
  • Dansk
  • Deutsch
  • eesti
  • English
  • Español
  • Français
  • Gaeilge
  • Hrvatski
  • Italiano
  • Kiswahili
  • Latviešu
  • Lietuviškai
  • Magyar
  • Nederlands
  • Norsk
  • Oʻzbekcha
  • Pilipino
  • Polski
  • Português (BR)
  • Português (PT)
  • Română
  • shqip
  • Slovenčina
  • Slovenščina
  • suomi
  • svensk
  • Tiếng Việt
  • Türkçe
  • Ελληνικά
  • Български
  • Қазақ
  • Македонски
  • Pусский
  • српски
  • Українська
  • ‏עברית‏
  • العربية
  • فارسی
  • اردو
  • বাংলা
  • हिंदी
  • ગુજરાતી
  • ಕನ್ನಡ
  • मराठी
  • தமிழ்
  • తెలుగు
  • മലയാളം
  • ภาษาไทย
  • 简体中文
  • 繁體中文
  • 日本語
  • 한국어
  • WhatsApp Web
  • Vipengele
  • Pakua
  • Usalama
  • Maswali Yanayoulizwa Sana
  • Pakua
  • Vipengele
  • Usalama
  • Maswali Yanayoulizwa Sana
  • Kuwa karibu

Ni jinsi gani tunaweza kukusaidia?

Unaweza kuperuzi mada hapo chini ili kupata kile unachokitafuta.
Windows PhoneUsalama na Faragha

Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho

Faragha na usalama ziko kwenye DNA yetu, ndiyo sababu tuna ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho. Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho ukiwepo, jumbe, picha, video, jumbe za sauti, nyaraka, sasisho za hadhi na simu zako zinalindwa ili zisiingie kwenye mikono isiyofaa.


Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho wa WhatsApp unahakikisha kuwa wewe tu na mtu unayewasiliana naye mnaweza kusoma jumbe zilizotumwa, na hakuna mtu katikati, hata WhatsApp. Jumbe zako zimehifadhiwa na kufuli, mpokeaji na wewe tu ndiyo wenye funguo maalum zinazohitajika kufungua na kusoma jumbe zako. Kwa ulinzi zaidi, kila ujumbe unaoutuma una kufuli na ufunguo wa kipekee. Yote haya hutokea kiotomatiki. Hakuna haja ya kuwasha mipangilio au kuweka soga maalum za siri ili kupata jumbe zako.

Muhimu: Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho umewezeshwa wakati wote. Hakuna njia ya kuzima ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho.

Skrini ya “Thibitisha Msimbo wa Usalama” kwenye maelezo ya mwasiliani ni nini?

Kila moja ya soga zako ina msimbo wa usalama unaotumiwa kuthibitisha kuwa simu na jumbe unazotuma kwenye soga zimefumbwa mwisho-kwa-mwisho.

Kumbuka: Mchakato wa uthibitisho ni wa hiari na unatumiwa tu kuthibitisha kuwa jumbe unazotuma zimefumbwa mwisho-kwa-mwisho.

Msimbo huu unapatikana kwenye skrini ya maelezo ya mwasiliani, kama msimbo wa QR pamoja na namba ya tarakimu-60. Misimbo hii ni ya kipekee kwa kila soga na inaweza kulinganishwa kati ya watu katika kila soga ili kuthibitisha kwamba jumbe unazotuma kwenye soga zimefumbwa mwisho-kwa-mwisho. Misimbo ya usalama ni matoleo ya wazi yenye kifunguo maalum kinachoshirikishwa kati yako - na usiwe na wasiwasi, sio kifunguo halisi, hiyo huwekwa kama siri.

Kuthibitisha kuwa soga imefumbwa mwisho-kwa-mwisho

  1. Fungua soga.
  2. Gusa jina la mwasiliani kufungua skrini ya maelezo ya mwasiliani.
  3. Gusa Ufumbaji kutazama msimbo wa QR na namba ya tarakimu-60.

Ikiwa wewe na mwasiliani wako mko karibu, mmoja wenu anaweza kukagua msimbo wa QR wa mwingine au kuangalia ili kulinganisha namba ya tarakimu-60. Ikiwa unasoma msimbo wa QR, na msimbo huo ni sawa, alama ya kijani itaonekana. Kwa kuwa ni sawa, unaweza kuwa na uhakika hakuna mtu anayeingilia kati ya jumbe zako au simu.

Ikiwa misimbo haifanani, kuna uzekano kuwa unakagua msimbo wa mwasiliani tofauti, au namba ya simu tofauti. Ikiwa mwasiliani wako amesakinisha tena WhatsApp au amebadili simu, tunapendekeza urejeshe msimbo kwa kutuma ujumbe mpya na kisha kagua msimbo.

Jifunze zaidi kuhusu misimbo ya usalama kwenye makala hii.

Ikiwa wewe na mwasiliani wako hamko karibu, waweza mtumie namba ya tarakimu-60. Mjulishe mwasiliani wako kwamba mara tu apokeapo msimbo wako, anapaswa kuandika na kisha kuilinganisha na namba ya tarakimu-60 inayoonekana kwenye skrini ya maelezo ya mwasiliani chini ya Ufumbaji. Kwa Android, iPhone na Windows Phone, unaweza kutumia funguo la Sambaza kutoka skrini ya Thibitisha Msimbo wa Usalama ili kutuma namba ya tarakimu-60 kupitia SMS, barua pepe, nk.

Jumbe zangu na simu na biashara zimefumbwa mwisho-kwa-mwisho?

Jumbe na simu zote za WhatsApp zimelindwa na ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho. Ni muhimu kukumbuka, hata hivyo, kuwa unapowasiliana na biashara, watu wengi katika biashara hiyo wanaweza kutazama jumbe zako. Biashara inaweza kutumia kampuni nyingine kusimamia mawasiliano yao - kwa mfano, kuhifadhi, kusoma au kujibu jumbe zako.

Biashara unayowasiliana nayo ina jukumu la kuhakikisha kwamba inashughulikia ujumbe wako kwa mujibu wa sera yake ya faragha. Kwa habari zaidi, tafadhali wasiliana na biashara hiyo moja kwa moja. Jifunze zaidi kwenye makala hii kuhusu ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho kwa jumbe za biashara.

Kwa nini WhatsApp inatoa ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho na ina maana gani kwa kuwaweka watu salama?

Usalama ni muhimu kwa huduma WhatsApp inayotoa. Tulikamilisha utekelezaji wa ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho mwaka wa 2016 kwa jumbe zote na simu kwenye WhatsApp ili kusiwe na mtu, hata sisi, anayepata maudhui ya mazungumzo yako. Tangu wakati huo, usalama wa kidijitali umekuwa muhimu zaidi. Tumeona mifano mingi ambapo wahalifu wadakuzi walipata kiasi kikubwa cha data za kibinafsi kinyume na sheria na kutumia vibaya teknolojia ili kuwaumiza watu na maelezo yao yaliyoibiwa. Kwa hiyo kama tulivyoanzisha vipengele vingi – kama simu ya video na Hadhi – tumeongeza ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho kwa vipengele hivi pia.

WhatsApp haina uwezo wa kuona maudhui ya jumbe au kusikiliza simu kwenye WhatsApp. Hiyo ni kwa sababu ufumbaji na ufichuaji wa jumbe zilizotumwa kwenye WhatsApp hutokea kwenye kifaa chako. Kabla ya ujumbe kuondoka kwenye kifaa chako, umehifadhiwa na kufuli la siri, na mpokeaji pekee ndiye ana ufunguo. Zaidi ya hayo, funguo zinabadilika kwa kila ujumbe unaotumwa. Wakati wote haya yanatokea nyuma ya matukio, waweza thibitisha kuwa mazungumzo yako yanalindwa kwa kuangalia uthibitisho wa msimbo wa usalama kwenye kifaa chako. Unaweza kupata maelezo zaidi jinsi hii inavyofanya kazi katika karatasi nyeupe.

Kwa kawaida, watu wameuliza ni nini maana ya ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho kwa utekelezaji wa sheria. WhatsApp inathamini kazi ambayo inafanywa na wakala za utekelezaji wa sheria kwa kuwaweka watu salama duniani kote. Kwa umakini tuna tathmini, kuthibitisha na kuitikia maombi ya watekelezaji wa sheria kulingana na sheria na sera husika, na tunatoa kipaumbele kwa maombi ya dharura. Kama sehemu ya jitihada zetu za elimu, tulichapisha habari kwa ajili ya utekelezaji wa sheria kuhusu maelezo machache ambayo tunakusanya na jinsi wanavyoweza kuyaomba kutoka kwa WhatsApp, unaweza kusoma hapa.

Kujifunza zaidi kuhusu usalama kwenye WhatsApp, tafadhali tembelea Usalama wa WhatsApp.

Makala hii ilikufaidi?
NdiyoLa
Kwanini makala hii haikukufaidi?
  • Makala hii ilikuwa na mkanganyiko
  • Makala hii haikujibu swali langu
  • Suluhisho sio sawa
  • Sipendi kipengele au sera
Asante kwa maoni yako
Mwanzo wa Maswali Yanayoulizwa Sana

WhatsApp

  • Vipengele
  • Usalama
  • Pakua
  • WhatsApp Web
  • Biashara

Shirika

  • Kuhusu
  • Kazi
  • Kituo cha Bidhaa
  • Kuwa karibu
  • Blog
  • Hadithi za WhatsApp

Pakua

  • Mac/PC
  • Android
  • iPhone
  • Windows Phone

Msaada

  • Maswali Yanayoulizwa Sana
  • Twitter
  • Facebook
2019 © WhatsApp Inc.
Faragha na Masharti