Wakati mwingine, unaweza kuona ujumbe hapo juu badala ya uliyotumiwa kutoka kwa mwasiliani. Kutokana na ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho, huenda ukahitaji kusubiri ujumbe wa mtufulani ufikie kwa sababu simu yao inahitaji kuwa mtandaoni ili kukufumbulia ujumbe kwa usahihi. Hii inaweza kutokea kwa kawaida ikiwa wewe au mtu unayepiga soga naye alisakinisha upya WhatsApp hivi karibuni.
Ili kuharakisha mchakato huu, unaweza kujaribu kumwuliza mtu unayemtumia ujumbe afungue WhatsApp kwenye simu yao.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali soma makala hii kuhusu ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho na makala hii kuhusu ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho kwa jumbe za kibiashara.