Unaweza kufuta jumbe za kila mtu au zako tu.
Kufuta jumbe za kila mtu
Kwa kufuta jumbe za kila mtu kunakukubalia kufuta jumbe maalum uliyotuma kwa soga ya kikundi au kibinafsi. Hii ina faida ikiwa ulituma ujumbe kwa soga isiyo sawa au kama ujumbe uliotuma una makosa.
Jumbe unazofuta za kila mtu zitabadilishwa na _“Ujumbe huu ulifutwa”_ kwenye soga za wapokeaji wa soga zako (*). Pia, ukiona _"Ujumbe huu ulifutwa"_ kwenye soga, inamaanisha kwamba mtumaji alifuta ujumbe wa kila mtu.
Kufuta jumbe za kila mtu:
- Fungua WhatsApp na nenda kwenye soga iliyo na ujumbe unayotaka kufuta.
- Gusa na shikilia ujumbe > chagua Futa
kutoka kwenye menyu. Kwa hiari, chagua ujumbe zaidi ili kufuta jumbe nyingi kwa mara moja.
- Ukiulizwa, gusa Zaidi
> chagua Futa kutoka kwa menyu.
- Gusa Futa
> Futa kutoka kwa Kila Mtu.
Kumbuka:
- Ili jumbe zifutwe kwa ufanisi kwa kila mtu, wewe na mpokeaji wako lazima mtumie toleo la karibuni la WhatsApp kwa Android, iPhone au Windows Phone.
- (*) Ikiwa wewe na wapokeaji hawatumii toleo la karibuni la WhatsApp kwa Android, iPhone au Windows Phone, kipengele hiki hakitawezeshwa.
- Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe kabla haijaufutwa au kama ufutaji haukufanikiwa.
- Hautaarifiwa kama ufutaji wa ujumbe kutoka kwa kila mtu haukufanikiwa.
- Una saa moja tu baada ya kutuma ujumbe kutimiza Futa kutoka kwa Kila Mtu.
Kujifutia jumbe
Kufuta jumbe zako kunakuruhusu kufuta nakili ya jumbe ulizotuma au kupokea kutoka kwa simu yako. Hii haina athari kwenye soga za wapokeaji wako. Wapokeaji wako bado wataona jumbe katika skrini yao ya soga. Kujifutia jumbe:
- Fungua WhatsApp na nenda kwenye soga iliyo na ujumbe unayotaka kufuta.
- Gusa na shikilia ujumbe > chagua Futa
kutoka kwenye menyu. Kwa hiari, chagua ujumbe zaidi ili kufuta jumbe nyingi kwa mara moja.
- Ukiulizwa, gusa Zaidi
> chagua Futa kutoka kwa menyu.
- Gusa Futa
> Futa yangu.
Kumbuka: Tafadhali elewa kwamba hatuwezi kufuta jumbe zako kwa vile sisi hatuhifadhi jumbe kwenye seva zetu mara tu zinazopokelewa.
Jifunze kufuta jumbe kwenye: Android | Windows Phone