Ili kutofautisha kati ya akaunti ya kibinafsi na akaunti ya biashara, unaweza kuangalia jalada la mwasiliani wako kuona aina gani ya akaunti waliyonayo. Ikiwa wana akaunti ya biashara, utaona moja ya yafuatayo yakioorodheshwa kwenye jalada:
Kumbuka: Ikiwa utaona akaunti ya biashara ambayo imeandikwa kama "Imethibitishwa" au "Imehakikishwa", basi tafadhali sasisha programu kuona aina za akaunti za biashara za hivi karibuni.
Tunakupa pia zana unazohitaji kudhibiti uzoefu wako na biashara. Unaweza kuzuia akaunti za biashara na kuziripoti wakati wowote, ndani ya soga (fungua soga > gusa Hiari zaidi > Ripoti au Zuia).
Kumbuka: "Akaunti rasmi ya biashara" haionyeshi kuwa WhatsApp inaidhinisha biashara hii.