Kufuta soga
Kufuta soga kunakuruhusu kufuta soga kutoka kwa tab ya Soga.
Kufuta soga ya kibinafsi
- Kwenye tab ya Soga, telezesha upande wa kushoto kwenye soga unayotaka kufuta.
- Gusa Zaidi > Futa Soga > Futa Soga.
Mbadala, kwenye tab ya Soga, gusa Hariri kwenye kona ya juu upande wa kushoto > Chagua soga unayotaka kufuta > Gusa Futa kwenye kona ya chini upande wa kulia > Futa Soga.
Kufuta soga ya kikundi
Kufuta soga ya kikundi, kwanza unahitaji kuondoka kwenye kikundi, kisha unaweza kufuta soga hiyo.
- Kwenye tab ya Soga, telezesha upande wa kushoto kwenye soga ya kikundi unayotaka kufuta.
- Gusa Zaidi > Ondoka kwenye kikundi > Ondoka kwenye kikundi.
- Kwenye tab ya Soga, telezesha upande wa kushoto kwenye soga ya kikundi tena > Futa Kikundi > Futa Kikundi.
Kufuta soga zote kwa wakati mmoja
- Nenda WhatsApp Mipangilio > Soga > Futa Soga Zote.
- Ingiza namba yako ya simu > gusa Futa Soga Zote. Soga za kibinafsi zitafutwa kutoka kwenye tab ya Soga. Soga za kikundi, hata hivyo, bado zitaonekana kwenye tab ya Soga, na bado utakuwepo.
Kufuta soga
Kufuta soga kunakuruhusu kufuta jumbe zote kwenye soga. Soga bado itaorodheshwa kwenye tab ya Soga.
Kufuta soga ya kibinafsi au kikundi
- Kwenye tab ya Soga, fungua soga unayotaka kufuta.
- Gusa Zaidi > Futa Soga.
- Gusa Futa zote isipokuwa zilizo na nyota au Futa jumbe zote.
Kufuta soga zote kwa wakati mmoja
- Nenda WhatsApp Mipangilio > Soga > Futa Soga Zote.
- Ingiza namba yako ya simu > gusa Futa Soga Zote. Hii itafuta jumbe zote kwenye soga yako. Soga bado zitaorodheshwa kwenye tab ya Soga.
Jifunze jinsi ya kufuta soga kwenye: Android | Windows Phone