Ni lazima uwe mtawala wa kikundi kuongeza au kuondoa washiriki kutoka kwenye kikundi kilichopo. Kikundi kinaweza kuwa na washiriki 256.
Kuongeza washiriki
Kuongeza mshiriki:
- Nenda kwenye kikundi kwenye WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Mbadala, bonyeza kwa muda kikundi kwenye tab ya Soga > gusa maelezo ya kikundi.
- Gusa ongeza mshiriki (+) .
- Mtafute au chagua mwasiliani wa kuongeza kwenye kikundi.
- Gusa ndiyo.
Kuondoa washiriki
Kuondoa mshiriki:
- Nenda kwenye kikundi kwenye WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Mbadala, bonyeza kwa muda kikundi kwenye tab ya Soga > gusa maelezo ya kikundi.
- Bonyeza kwa muda mshiriki unayetaka kumwondoa.
- Gusa ondoa {mshiriki} > ndiyo.