Elewa ujumbe ukiwa umesambazwa
Jumbe zilizo na lebo ya “Ilisambazwa” zitakusaidia kuamua kama rafiki au ndugu ameandika ujumbe huo au kama umetoka kwa mtu mwingine. Ujumbe unaposambazwa kutoka kwa mtumiaji mmoja kwa mwingine zaidi ya mara tano, hii inaashiriwa na ikoni ya mishale miwili . Ikiwa hauna uhakika ni nani aliyeandika ujumbe wa awali, angalia mara mbili kupata ukweli. Ili kujifunza zaidi kuhusu kusambaza jumbe, tafadhali somamakala hizi.
Angalia picha na media kwa makini
Picha, sauti, na video zinaweza kuhaririwa ili kukupoteza. Angalia vyanzo vya habari vya kuaminika ili uone kama hadithi hiyo imeripotiwa mahali pengine. Hadithi ikiripotiwa katika maeneo mengi, inawezekana zaidi kuwa kweli.
Angalia kama ujumbe unaoonekana tofauti
Jumbe nyingi au viungo vya tovuti unazopokea zilizo na uwongo au habari za bandia zina makosa ya herufi. Angalia ishara hizi ili uweze kuangalia kama habari hii ni sahihi. Kujifunza zaidi kuhusu jumbe za hila, soma makala hii.
Zingatia uchunguzi
Jihadhari na habari ambazo zinathibitisha imani yako ya awali na chunguza ukweli kabla ya kushirikisha habari. Hadithi ambazo zinaonekana vigumu kuamini mara nyingi sio za kweli.
Habari bandia mara nyingi huenea sana
Hata kama ujumbe unashirikishwa mara nyingi, hii haifanyi kuwa kweli. Usisambaze ujumbe kwa sababu mtumaji anakuhimiza kufanya hivyo. Ikiwa unapoona kitu ambacho ni bandia, mwambie mtu aliyekutumia na uwaombe wathibitishe maelezo kabla ya kushirikisha. Ikiwa kikundi au mwasiliani anatuma habari bandia kila mara, mripoti. Kujifunza jinsi ya kuripoti mwasiliani au kikundi, tafadhali soma makala hii.
Thibitisha na vyanzo vingine
Ikiwa bado haujui kama ujumbe ni wa kweli, tafuta mtandaoni kwa ukweli na angalia maeneo ya habari ya kuaminika ili uone mahali ambapo hadithi imetoka. Ikiwa bado una wasiwasi, waulize wahakiki wa ukweli au watu unaowaamini kwa habari zaidi.
Muhimu Ikiwa unajisikia kuwa wewe au mtu mwingine yuko katika hatari ya kihisia au kimwili, tafadhali wasiliana na mamlaka yako ya kutekeleza sheria. Mamlaka za kutekeleza sheria za mitaa zina vifaa vya kusaidia katika kesi hizi.